Mahafali ya nne ya shule ya secondari ya WAMA NAKAYAMA
Tuesday, December 13, 2016 By Everada Benjamini WAMA Advocacy and Communications Department

Akiongea katika sherehe za mahafali hayo  Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete  alisema Shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama ilianzishwa  ili kutoa mchango  katika Juhudi za Taifa za kumkomboa mwanamke  kwa kuwapatia fursa za  elimu bora ya sekondari watoto wa kike wanaotoka katika mazingira magumu wakiwemo yatima.Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete Akiongea kwenye mahafali ya kidato cha nne katika shule ya WAMA Nakayama

 “Taasisi ya WAMA inatambua na inalenga kuchangia katika utekelezaji wa Sera ya Elimu ya Taifa inayowataka wadau mbalimbali kusaidia kuongeza fursa za elimu kwa watoto wa kike, ili kutoa mchango endelevu tulitambua kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na shule zetu, kwa kuzingatia hilo ndipo mwaka 2010 tulianzisha shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama na hatimaye 2016 tulianzisha shule nyingine ya WAMA-Sharaf iliyopo katika Manispaa ya Lindi.

 Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete  aliongeza kwa kusema moja ya mikakati ambayo Taasisi ya WAMA tumekuwa tukitekeleza ni kuchangia katika kupunguza na ikiwezekana kuondoa kabisa uwiano mbaya wa kijinsia tuliorithi kutoka utawala wa kikoloni. Watoto wakike wameachwa nyuma kielimu kwa ujumla na haswa elimu ya sayansi, hisabati na teknolojia, ukilinganisha na wenzao wa kiume. Ni muhimu sasa tuachane na desturi zinazowanyima watoto wengi wakike nafasi ya kwenda shuleni kwa  kuwaona kama ni watu wa kusaidia kazi za nyumbani na kulea familia. Ni lazima sote tukemee na kuacha kuwatumia watoto wetu wa kike kama chanzo cha kipato kupitia mahari wanayotoza wazazi bila kujali maslahi yao na maisha yao ya baadae.wahitimu wa kidato cha nne kutoka shule ya Wama Nakayama

 

 

Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete aliongeza pia kwa kusema nikiwa mwalimu kwa zaidi ya miaka Ishirini nimeona kwamba hakuna tofauti za uwezo wa kimasomo kati ya watoto wakike na wakiume. Hivyo mtoto wakike anachohitaji ni fursa tu sawa na ya yule mwenzake wa kiume ili naye aweze kufanikiwa na ili mtoto wa kike aweze kupata mafanikio katika masomo yake ni muhimu kumjengea mazingira wezeshi ya kusomea na kuishi. Ndiyo maana tuliamua kuwajengea shule yenye mahitaji yote ya kupata elimu bora na pia kuepuka vishawishi mbalimbali vinavyoweza kupelekea kukatisha masomo.

 

Mama Kikwete alimshukuru Mgeni Rasmi, wadau wote pamoja na wageni wote, wanakijiji, walimu wote na wafanyakazi wasio walimu kwa kuhudhururia sherehe hiyo ya Mahafali iliyofanyika katika kijiji cha Nyamisati wilayani Kibiti. Pia Mwenyekiti wa WAMA aliwapongeza wahitimu wa kidato cha nne kwa kutambua thamani ya fursa ya Elimu waliyoipata, na kuwasisitizia kuyashika mazuri yote walifundishwa wakiwa shuleni kwani safari ya Elimu bado ni ndefu kwao.

 Mwakilishi wa Balozi wa JapanMwakilishi toka ubalozi wa Japan akisoma hotuba ya Balozi wa Japan hapa nchini alisema shule hii iliweza kuanzishwa kwa  msaada kutoka kwa Bw. Nakayama wa Japan ambaye alichangia hela za ujenzi wa shule.  Aliongeza kwa kuwaambia wahitimu kuwa japo wamefanikiwa kuhbitimu masomo yao ya kidato cha nne na wamejifunza mengi wakiwa hapo shuleni ila wajue ilo lisiwe lengo lao kuu kwasababu safari yaoo kimasomo bado ni ndefu sana, na wakumbuke kluwa juhudi zao katika kuendelea na masomo ndio ufunguo wa maendeleo ya taifa kwani Vijana ndio taifa la kesho.

 

 

 Shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama iliyopo  Nyamisati, Kibiti katika Mkoa wa Pwani ilianza rasmi mwaka 2010. Shule inasaidia wasichana yatima na waliotoka katika mazingira hatarishi kutoka mikoa yote Tanzania bara na visiwani. Jumla ya wanafunzi wa kike 79 wamehitimu kidato cha nne mwezi Novemba mwaka huu katika michepuo ya Biashara, Sayansi na Sanaa.

 

Terms of Use | Privacy Policy | SitemapCopyright © 2010 - 2018 WAMA Foundation, All Rights Reserved