NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA KWA MWAKA 2016 WAMA NAKAYAMA NA WAMA SHARAF
Event Location:
KIbiti Rufiji na Mitwero Manispaa ya Lindi
Event Date:
12 November, 2015

Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inatangaza nafasi za kidato cha kwanza kwa wasichana katika Shule zake mbili za Sekondari:

 (1)   Shule ya Sekondari WAMA -  Nakayama  iliyopo Kijiji cha Nyamisati Wilaya ya Kibiti , Mkoa wa Pwani:

(2)   Shule ya Sekondari ya WAMA- Sharaf iliyopo Mitwero katika  Manispaa ya Lindi

 WAMA ni Taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na Mhe. Mama Salma Kikwete ili kusaidia maendeleo ya wanawake na watoto. WAMA inaendesha shule hizi maalum kwa ajili ya watoto yatima na wanaotoka katika mazingira magumu. Hata hivyo, WAMA inatoa fursa chache kwa wanafunzi wengine ambao wazazi wao wana uwezo wa kulipia ili kuongeza uwezo wa kusaidia watoto wengi zaidi.

Tunafurahi kutoa fursa hii kwa wasichana ambao wataweza kulipia ada kwa kidato cha kwanza katika shule zote mbili kwa mwaka 2016.

Fomu za kujiunga  zimeambatanishwa hapo chini au unaweza  kuzipata  katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Dar es Salaam zilizopo Kawe karibu na Hoteli ya Picolo Beach

Kwa wakazi  wa Lindi fomu zinapatikana katika Ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) tawi la Lindi zilizopo  katika makutano ya Barabara ya Karume na Amani , Kiwanja no.11 kitalu B karibu na  Ofisi za  Magereza  za Mkoa wa Lindi

Kwa Dar es Salaam mtihani wa kujiunga na shule zote mbili utakaotolewa na shule yetu utafanyika Alhamisi Novemba 12, 2015 katika Shule ya Sekondari Jangwani.

Kwa Lindi mtihani wa kujiunga na shule zote mbili utakaotolewa na shule yetu utafanyika  Alhamisi Novemba 19, 2015 katika  Chuo cha VETA Lindi.

Mwanafunzi anatakiwa arudishe fomu pamoja na risiti ya malipo katika ofisi za Taasisi ya WAMA au kwa kutumia barua pepe: info@wamafoundation.or.tz, mbugunimwajuma@gmail.com na alimindria66@yahoo.com.  Mwisho wa kurudisha fomu ni Jumatano tarehe 11 Novemba, 2015.

Terms of Use | Privacy Policy | SitemapCopyright © 2010 - 2018 WAMA Foundation, All Rights Reserved