NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KATIKA SHULE YA SEKONDARI WAMA NAKAYAMA
Event Location:
Kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji
Event Date:
2 March, 2015

Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) inatangaza nafasi za kidato cha Tano mwaka 2015 kwa wasichana katika Shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama iliyopo Nyamisati Wilaya ya Rufiji, Mkoa wa Pwani.

WAMA ni Taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na Mhe. Mama Salma Kikwete ili kusaidia maendeleo ya wanawake na watoto. WAMA inamiliki na kuendesha shule Maalum kwa ajili ya watoto yatima na wasio na uwezo.

Hata hivyo kwa sasa tumeanza kupokea wanafunzi wachache watakaolipia ili kusaidia uendelevu wa shule. Mtihani wa kujiunga utakaotolewa na shule yetu utafanyika Machi 21, 2015 katika Shule ya Sekondari Jangwani-Dar es Salaam.

Mwanafunzi anatakiwa arudishe fomu pamoja na risiti ya malipo katika ofisi za Taasisi ya WAMA au kwa kutumia barua pepe: info@wamafoundation.or.tz.  Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 18 Machi, 2015.

Shule ni ya bweni ya wasichana na ina mazingira mazuri ya kujisomea pamoja vifaa muhimu vya kujifunzia.

Kwa Mawasiliano zaidi

Piga Namba:  022-2126516, 0754-086896, 0754- 439183,

Barua pepe: info@wamafoundation.or.tz

Tafadhali  fungua fomu za kujiunga hapo chini

Terms of Use | Privacy Policy | SitemapCopyright © 2010 - 2018 WAMA Foundation, All Rights Reserved